Utangulizi

Tangu nakumbuka nilikuwa nikiishi karibu na wanyama. Nilipokuwa mdogo sana tuliishi mashambani. Baadaye tukahamia jijini, Budapest. Kisha vile nimekuwa mkubwa kidogo, nikapeleka nyumbani wanyama maalum aina mbalimbali, kama samaki, ndege ndogo, kasuku, halafu chura, kobe, nyoka, jusi, nge, au kinda mwenye mbawa kuvunjikiwa, na ndege mwingine aliyekaa bafuni, pia mbwa saba nimeowalisha kutoka chupa. Siku moja nikarudi nyumbani na  paka mchanga wa porini na kumlea chumbani hadi amekua. Wazazi wangu wapendwa walishtuka vibaya. Tusishangae kuwa walitulia moyoni nilipotoka ghorofa ya nne na kuhamia mashambani.

Huko sasa nilikuwa na nafasi ya kufugia wanyama wakubwa, kama farasi, nyati, mbuzi, kondoo, punda na ng’ombe. Na vilevile kuku, bata, paka na mbwa. Wakati uleule kwa muda mrefu nilifanya kazi katika shamba la wanyama yaani zoo iliyoko karibu kwangu.

Wakati huu nafanya kazi nyumbani, nalea farasi.

Nimegundua kuwa ”maradhi” yangu ya kupenda wanyama yarithika: binti yangu akaniambia kuwa anataka kufuga paka. Alipotaja hii tayari tulikuwa na paka watano wadogo wakirarua na kuharibu nyumba yetu. Binti yangu amezaliwa kwenye nyumba inayomfaa kabisa, maanake hata mimi natamani paka tangu niwe mtoto.

Gosztonyi Fanni  na  Dóra

bengáli macska tenyésztő          bengal cat breeder

paka wa kibengali

fanni 2016. January 1.

Írta: